Jumapili 26 Oktoba 2025 - 18:50
Sheikh Naeem Qassem Kufanya Mzungumzo na kituo cha Al-Manar

Hawza/ Sheikh Naeem Qassem, usiku wa leo, kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu achukue wadhifa wa Ukatibu Mkuu, atakuwa mgeni katika kituo cha Al-Manar.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, likinukuu kutoka kwenye kituo cha Al-Manar, Sheikh Naeem Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, siku ya leo Jumapili saa 2:30 usiku, kutokana na kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ktimiza mwaka mmoja tangia achukue wadhifa wa Ukatibu Mkuu, atakuwa mgeni rasmi katika kituo cha Al-Manar.

Katika mahojiano haya, Sheikh Qassem atazungumzia hali ya sasa na uvamizi unaofanywa utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon na muqawama, uongozi wake katika vita na mabadiliko ya kisiasa na ya kijeshi.

Sheikh Qassem pia atazungumzia kuhusiana na uchaguzi wa wabunge ujao na mambo yanayopendekezwa, uhusiano wa Hizbullah na Rais pamoja na Waziri Mkuu katika muktadha wa mgogoro wa kisiasa wa ndani, jalada la ujenzi upya katika maeneo ya kusini, vitongoji vya kusini na bonde la Bekaa, pamoja na nafasi ya serikali na Hizbullah.

Sheikh Qassem pia atatoa tathmini yake kuhusiana na mkutano wa Sharm el-Sheikh, matokeo na athari zake, changamoto za baadaye za Lebanon na eneo zima, na msimamo wa Hizbullah kuhusu mazungumzo yanayopendekezwa kwa ajili ya Lebanon.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha